Usipitwe na hizi...


Wednesday, 28 February 2018

Okwi avunja rekodi VPL

MSHAMBULIAJI wa Simba, Mganda Emmanuel Okwi amevunja rekodi ya ufungaji kwenye Ligi Kuu iliyowekwa msimu uliopita na Simon Msuva na Abdulrahman Musa baada ya kufikisha magoli 16 kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu.
Msuva aliyekuwa Yanga na Abdulrahman wa Ruvu Shooting walifunga magoli 14 kila mmoja na kuibuka wafungaji bora msimu uliopita.
Msuva kwa sasa anacheza klabu ya Difaa El Jadidi ya Morocco ambapo anafanya vizuri.
Okwi aliifikia rekodi hiyo kwenye mchezo wa juzi ambapo Simba ilishinda mabao 5-0 dhidi ya Mbao kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam baada ya kufunga mabao mawili kati ya hayo.
Hadi sasa Okwi bado anaendelea kuongoza kwenye orodha ya wafungaji wa msimu huu akiwa na mabao yake hayo 16 akifuatiwa na Obrey Chirwa wa Yanga mwenye mabao 11 huku John Bocco wa Simba akishika nafasi ya tatu ka mabao yake 10.
Mabao ya Simba dhidi ya Mbao yalifungwa na Shizza Kichuya (dakika ya 38), Emmanuel Okwi (dakika ya 41, 70), Erasto Nyoni (dakika ya 82) na Nicholas Gyan (dakika ya 87). Mbao haijawahi kupata ushindi dhidi ya Simba tangu ilipopanda Ligi Kuu msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment

Pages