Usipitwe na hizi...


Wednesday, 28 February 2018

UN: Mapigano yamezuia kusambaza misaada Ghouta,Syria

Kusitishwa kwa mapigano hayo kungesaidia kusambazwa kwa misaada ya kibinaadam sehemu hatarishi
Image captionKusitishwa kwa mapigano hayo kungesaidia kusambazwa kwa misaada ya kibinaadam sehemu hatarishi
Umoja wa mataifa umesema mapigano yanayoendelea Mashariki mwa mji wa Ghouta nchini Syria yamezuia kusambazwa kwa misaada licha kukubaliana kuwepo kwa usitishwaji wa mapigano kwa saa tano.
Kusitishwa kwa mapigano kulikwama siku ya Jumanne huku kila pande ikiilaumu nyingine kwa kuwa sababu.
Takriban watu sita wameuawa huku wengine wakijeruhiwa.
Umoja wa mataifa umezilaumu pande zote mbili kwa kukiuka makubaliano
Image captionUmoja wa mataifa umezilaumu pande zote mbili kwa kukiuka makubaliano
Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu imesema kusitishwa kwa saa tano hakutoshi kusambaza misaada, kwa sababu kupita kwenye vizuizi hutumia hata siku nzima.
Afisa mmoja wa umoja wa mataifa ameiambia BBC kuwa kilichohitajika ni kusitishwa mapigano kwa mwezi mzima.

No comments:

Post a Comment

Pages