SEHEMU YA SITA
Fimbo hiyo itibu kila ugonjwa
utakaosumbua kila mtu akuombaye msaada, taji hilo uwe
malkia wa ulimwengu mzima lakini hayo yote ni baada ya
kutimiza masharti haya nikupayo"
alinyamaza kwa muda kabla hajaendelea. Babu
alinitazama kwa jicho la huzuni. Sikujua ilikuwa hivyo
kwanini. Mimi nilitabasamu kumpa moyo babu kuwa
ningeyaweza yote ambayo ningeambiwa. Yule kiumbe wa
ajabu, alikohoa kisha alizungumza.
"masharti hayo ni kwamba tunamuhitaji yule mpenzi wako
kama kafara. Ndugu jamaa na raiki zako hapa Gamboshi
wanywe damu yake na kuila nyama yake katika sikukuu
ya kukabidhiwa utawala wako" nilifahamu kuwa huyu
kumbe alikuwa akimaanisha Jordan. Nilinyamaza
kumsikiliza. Aliendelea
" Pia usiongee na mtu yeyote kwa siku nzima mara
utakapoamka leo ukitoka hapa Gamboshi. Usithubutu
kulowa maji kwa muda wa siku tatu ikiwa mvua ama
kuoga kufanya hivyo utatoa utawala wako katika koo
nyingine na adhabu yako itakuwa ni kuongea milele na
kutoa siri zako ovyo kwa yeyote hata usiyemfahamu.
Wewe na maji mtakuwa maadui mpaka unakufa"
sikukubali haraka. Mkutano mzima ulikuwa kimya kusikia
kama ningekubali kufuata masharti ya kiumbe huyo wa
ajabu. nilinyamaza kimya kwa muda. Babu aliuinua uso
wake na kupaza sauti "Bella mjukuu wangu tunasubiri jibu
lako ili tuweze kutawanyika"
niliendelea kunyamaza. "na kama hutajibu leo, usitarajie
kuamka milele siku ya kesho ukitoka hapa Gamboshi"
nikaipata sauti yangu kwa uoga wa kitisho cha kiumbe
huyo wa ajabu nikasema. "nitatimiza kila ninalopaswa
kulitimiza" mkutano mzima ukalipuka kwa shangwe. Kila
mtu alifurahi sana, furaha ikazidi kupitiliza. Babu
alipongezwa kwa kuimaliza kazi, kazi ya kunikabidhi
mikoba. Kazi iliyomchukua muda mrefu kuikamilisha. Kazi
iliyopingwa na mama kwa muda mwingi, sasa ikawa
kama kumsukuma mlevi. Kile kiumbe kikapotea kikiwa na
furaha ya ajabu. Niliwaona wale wachawi wa Gamboshi
wakila na kunywa. Nilipotoka kitini na kwenda kujumuika
nao, nilistaajabu sana. Nilistaajabu kuona wakinywa damu
ya binadamu kwa furaha wakitafuna nyama ya mtu. Babu
alinipongeza kwa kuniambia kuwa "umefanya jambo zuri
sana" alinikabidhi nyama ya mtu ambayo niliikataa.
Sikuwa mzoefu ghafla kiasi hicho kuanza kula nyama ya
binadamu mwenzangu. Ila kutokana na jinsi ilivyochomwa
na babu alivyonilazimisha niinywe, nilijishangaa nikikakata
pande na kulitia mdomoni. Ama kweli ndio maana
tulikatazwa tusimle binadamu mwenzetu. Nyama ilikuwa
ni tamu kupitiliza. Hakuna mnyama yeyote iwe wa
kufugwa ama wa porini, aliupita utamu wa Binadamu. ila
babu alilinisisitiza sana nisifanye kosa katika masharti
niliyopewa
"nitakuwa sina jinsi ya kukusaidia katika hili ukifanya
kosa. Kwa kuwa umekubali mwenyewe" aliniambia
"Hakikisha unatimiza yote uliyoambiwa"
nilimkubalia babu huku moyoni nikiwa na jambo
ninalolifikiria. Mawazo yangu moyoni, hayakuwa juu ya
utawala wala wadhifa niliokabidhiwa. Mawazo yangu
yalikuwa kwa Jordani. Sura ya Jordani ilikuja kwenye akili
yangu na kunipotea kila nikikumbuka sharti nililopewa na
yule kiumbe. Jordan mwanaume niliyempenda kuliko kitu
chochote katika hii dunia. Sikutaka nimpoteze Jordani, si
kwenye kifo hata kwa mwanamke mwingine. Ndio maana
nikachuma bibo kutoka katika mti wa mkorosho
nyumbani, nikajichora jina lake 'JORDANI' kwenye mkono
wangu kwa kutumia utovu wake. Nilimpenda sana Jordan
baada ya mama yangu. Sharti hilo ndio nililiona lingekuwa
gumu kuliko yote niliyopewa hapo Gamboshi. Nikiwa bado
Gamboshi kila mtu alipepesuka kwa ulevi wa furaha.
Tulirudi lile eneo ambalo mimi na babu tulibadilishia nguo.
Nilizivua zile nguo abazo zilikuwa maalumu kwa ajili ya
shughuli ile ya kukabidhiwa mamlaka na nguvu, kisha
nikazivaa zile nilizokuja nazo. Babu akanieleza kitu cha
ajabu sana aliniambia
"Bella nimeitumikia Gamboshi kwa muda mrefu sasa.
Inabidi nilipe fadhila kwa kila jambo walilonifanyia nikiwa
duniani. Miaka yangu ya kuishi duniani ilishakwisha muda
mrefu sana, ila niliongezewa muda wa kuwakabidhi wewe,
urithi mamlaka yangu. Sasa ninatakiwa kuja kuishi huku
Gamboshi nikipewa nafasi nyingine baada ya wewe
kuikaimu nafasi yangu. Nitaishi huku Gamboshi mpaka
wakati wangu wa kuishi utakuwa umekwisha kabisa"
nilishangaa sana. Sikujuwa kama kumbe kuna miaka ya
kuishi duniani na miaka ya kuja kuishi huku Gamboshi.
Nilimuuliza babu hii inakuwaje. "sijaelewa kabisa" babu
alinieleza
"kwa sisi huku Gamboshi tunaishi miaka nusu kwa nusu
nikimaanisha kama duniani ulitakiwa kuishi miaka
themanini, utaishi arobaini duniani arobaini huku
Gamboshi. Kwa hivyo wakati mimi naanza kuhiji huku
Gamboshi nilipimwa na kugundulika nina miaka mia na
nne ya kuishi duniani" nilishituka, macho yakanitoka pima.
babu akaendelea
"hivyo ndio maana nimeishi miaka sitini duniani na
iliyobaki yote nitakuja kuishi huku Gamboshi"
hapo nikawa nimemuelewa babu. Tulipomaliza
kubadilisha nguo babu aliniambia kuwa nisimueleze mtu
yeyote, ila siku chache zijazo atalala usingizi wa milele
akiwa kitandani kwake. Hivyo nisishitushwe na hayo
yatakayotukia kwa sababu ni lazima yatukie.
Nilitamani kulia lakini alinieleza "mjukuu wangu mimi na
wewe tutakuwa tunaonana mara kwa mara hivyo
usiogope" nilijipa moyo kwa kutabasamu kinafki. Nilikuwa
nimeshamzoea Babu. Ubaya wake sikuuona tena na
nilimpenda sana. Nilihisi kuupenda uchawi zaidi kwa
kipindi hiko, ila kila nikifikiria kuila nyama ya mwanaume
nimpendaye, niliona ni jambo gumu sana kulitimiza. mimi
na babu tulitoka Gamboshi tukarudi katika ulimwengu wa
kawaida. Babu aliishi magomeni usalama mimi nilielekea
Sinza nyumbani nilipobakia mimi na Mzee Nyegezi baada
ya mama kufariki.
..........................
Nilijikuta nipo kitandani Mzee Nyegezi alikuwa
akiniamsha. Nilipiga ukunga mkubwa sana
"haiwezekaniiiiiiiii!!!" Mzee Nyegezi aliruka pembeni na
kuniacha. Niliendelea
"siwezi kumuua Jordani" nilipoamka kabisa niliuona
mshituko wa dhati wa Mzee Nyegezi.
aliniuliza "una tatizo gani" Nilinyamaza. Nilinyamaza kwa
kuwa nilikumbuka sharti nililopewa Gamboshi. "usiongee
na mtu yeyote mara kutapokucha baada ya kutoka hapa
gamboshi" sauti ya yule kiumbe aliyejitambulisha kama
Lucifer, ilijirudia kichwani mwangu. Mzee nyegezi
hakutoka hata nilipokuwa nimenyamaza muda wote.
Niliushika mdomo wangu wa uoga nikijiuliza kama, Mzee
nyegezi alisikia nilichoropoka, ama hakukitilia maanani.
"Bella una nini? Umeanza kupiga kelele muda mwingi
sana. Tangu usiku mimi sikulala kabisa" Aliposema hivyo
nilijiuliza, hivi mbona Gamboshi nilichukuwa muda mrefu
katika kila jambo lililotokea kule? sasa iweje Mzee
Nyegezi ahesabu kama ilikuwa ni siku moja tu?
nikajisahau nikamuuliza swali.
"kwani nimelala kwa muda gani?"
"sasa hivi ni saa tatu asubuhi na ulilala jana mapema
hata chakula cha usiku hukula"
nikakumbuka hapo hapo kuwa nimeshavunja sharti moja
wapo kati ya yale niliyopewa kule Gamboshi. Nililia sana
hata Mzee Nyegezi asijue nilikuwa nalilia nini. Nilimpiga
kikumbo mzee nyegezi na kuelekea chooni kunawa uso
huku nikiwa nalia. Chooni ndipo nilikutana na babun Babu
alikuwa akilia na yeye pia. Alilia machozi mfano wa damu.
Aliniuliza
"ina maana mjukuu wangu yote niliyofanya kwako
yamekuwa ni bure kabisa?"
nilikabwa na kitu kooni hata nikashindwa kuongea nililia
kwa uchungu ambao sikuwahi kuupata tangu nijitambue.
Nilimuomba babu msamahan "nisamehe babu. Naomba
uniombee anisamehe mkuu wa Gamboshi" Babu alinivunja
moyo kabisa, aliniambia. "tazama jinsi Gamboshi
ilivyohuzunika, tazama kwa macho yako" kwa kuwa ukuta
wa choo chetu ulikuwa mweupe sana ikawa kama sinema
nilipotazama aliponioneshea kwa kidole. Ilikuwa ni taswira
ya Gamboshi.
Mkuu wa Gamboshi ambaye ni yule Lucifer, alikuwa
amekasirika sana. Babu alinionesha hadi kwenye makazi
yake alipokuwa akiishi yeye lucifer. Kutokana na hasira,
alikuwa akibadilika kila mnyama. Moto ulimtoka mdomoni
kwa hasira iliyomzidi na kushindwa kujizuia kupunguza
hasira zake. Hakika nikagundua nimefanya makosa
makubwa sana.
babu alinieleza "kuanzia sasa umepokonywa utawala na
wadhifa wako wote umevuliwa kutoka Gamboshi.
Hutakuwa na nguvu zozote, bali utakuwa na uwezo kama
wa mchawi yeyote yule." babu alinyamaza kisha
aliniangalia kwa huzuni. Mimi nilikuwa nalia sana, hata
macho yalifumba kwa machozi. babu aliendelea "sijajua
mkuu atakupa adhabu gani ila amekasirika sana sina cha
kukueleza" babu akatoweka kabla sijamueleza chochote.
siku hiyo nikawa nimeianza vibaya. Mzee Nyegezi
hakuthubtu kuniuliza kitu kingine niliporudi chumbani na
kupishana naye kibarazani. Alikuwa akinitazama tu,
alipokuwa akielekea nje. Nilipokuwa chumbani, nilikaa
kimtegomtego, nikimtegea babu nikidhani labda ningesikia
ujio wake. Upepo ungevuma, kama siyo radi ingepiga
baada ya mngurumo wa kutisha. Nilitamani kujua
chochote kutoka Gamboshi. Niliumia sana kuukosa
utawala niliokabidhiwa. Nikamuona mzee Nyegezi ni mtu
mbaya sana kwangu. Nikamchukia kwa kuniamsha
asubuhi na kunifanya nizungumze. Kuzungumza kule
kulinifanya nivunje sharti. Moyo uliniuma kila nilipofikiria
kuona kuwa sharti dogo nililodhani ningeliweza, kumbe
hilo ndio lilikuwa gumu sana kwangu. Niliutamani tena
ukuu na uwezo niliokabidhiwa kutoka katika kiti cha urithi
wa babu. Mawazo yakanisonga, mawazo yakanifanya hata
nisahau kufanya mambo mengine. Kwa sababu ya
mawazo, nilisahau hata kula wala kupika. Kwa sababu ya
mawazo, sikujua nilijilaza kwa muda gani hapo kitandani
kichwa changu kikielea juu ya kidimbwi kidogo cha
machozi. Kwa sababu ya mawazo, mawazo yakawa
mawazo, nikapitiwa tena na usingizi. Niliamka saa nne ya
usiku, tena si kwa kupenda ni Mzee Nyegezi ndiye alikuja
kuniamsha. Alipatwa na wasiwasi jinsi nilivyolala. Nililala
tangu jana mapema, lakini nilichelewa kuamka.
Aliponiamsha saa sita mchana nilimuacha chumbani na
niliporudi chumbani niliendelea kulala mpaka sasa.
alizungumza na mimi kwa upole "Bella kama unaumwa
sema. Kukaa kimya si vizuri" mimi sikumjibu kitu.
Nilimchukia sana Mzee Nyegezi. Nilimuona Mzee Nyegzi
hakuwa akinitakia mema. Alining'ang'ania kunibembeleza
mpaka nilipoamua kuzungumza. "siumwi nipo sawa"
nilimjibu kwa dharau sana. Lakini hakuweka ukali katika
sauti yake. "sasa kwanini unalala lala oyo? Jana umelala
saa moja jioni. Nimekuja kukuamsha leo saa sita mchana,
nashitushwa kukukuta umelala tena. Umekula nini leo?"
niliendelea kumjibu kwa dharau nikibetua midomo yangu
kama shangingi.
"ningesikia njaa ningeamka kupika" aliendelea "najua
unajisikia vibaya kutokana na kifo cha mama yako,
hakuna ambaye hajaguswa nacho. Tafadhali Bella usiwe
mnyonge kiasi hicho nipo hapa kwa ajili yako" alitoa noti
tano za elfu kumi na kunipatia baada ya kunibusu.
Nilimsonya na kujilaza tena kitandani.
nikiwa nimejilaza huko, kile ambacho nilikuwa nikikisubiri
tangu mchana nilikisikia kikinijia. Ilikuwa ni sauti ya
upepo mkali sana. Mngurumo mkubwa wa radi, ulisikika
kila pande. Tetemeko la ardhi likatokea katika chumba
changu na kukipasua chumba changu katikati. Wakati
hayo yakitokea. Mlango wa chumba changu ukafunguliwa.
Alikuwa Mzee Nyegezi.
aliniambia "pipa halina maji hata kidogo, hakikisha
unayakinga haya ya mvua kisha urudi tena kulala" wakati
akiyaongea hayo, mimi nilikuwa nikipatazama pale
palipopasuka. Kulikuwa vile vile na moshi mzito ulikuwa
ukifuka kutoka katika shimo hilo. Nilikuwa nikimuangalia
Mzee Nyegezi, hakuonesha kama aliona kile ambacho
mimi nilikuwa nikitazama. Niljifanya kumskiliza kwa
makini na kumkubalia alichoniagiza.
Alipoondoka nilijiuliza. Nilijiuliza ina maana hakuona
kilichotokea chumbani kwangu? Chumba changu
kilipasuka na kuweka mfano wa bonde la ufa. Ndani yake
akatokea kiumbe aliyetisha sana. Nilianza kutetemeka
kwa uoga uliopitiliza. Kiumbe huyo alikuwa na uso wa
babu, Mzee Matonde. Babu alikuwa akilia machozi ya
damu. Sikujuwa machozi hayo yalikuwa yakimaanisha
nini. Mara kwa mara babu alikwa akilia hivyo. Alikuwa na
mwili wa mnyama. Babu alikuwa na mwili wa fisi, fisi
mwenye miguu mikubwa sana kama ya tembo. Fisi huyo
hakuwa wa kawaida. Alikuwa na mabawa kama ndege na
meno marefu kama ngiri. Shimoni alipotoka, kulikuwa
kukifuka moshi mzito sana. Moshi huo ulisindikizwa na
harufu kali ya uvundo. Joto la chumbani lilizidi na
kunifanya nihisi kama nipo karibu na moto mkali wa
jikoni. Nilivuja jasho japo sikujua lilikuwa ni jasho la
uwoga ama hili la joto kali.
Kiumbe kile kikapata sauti yake iliyotisha. "mjukuu
wangu" nikajuwa kuwa alikuwa ni babu
"kesho asubuhi utapata habari za msiba wangu. Lakini
hakikisha mwili wangu haufanyiwi maombi wala kuagwa
na watu wengi." nilishitushwa na habari hizo. Japo
nilikwishajua kiumbe yule ni babu, sikuwa na uhuru nafsini
mwangu. Alikuwa akitisha sana. Nilimuuliza
"kwanini hayo?" akaniambia "mimi nitakuwa sijafa ndiyo
sababu ya kukueleza ufanye hayo"
"sasa babu, mimi nitawezaje kuzuia watu wasiuage mwili
wako au wasiuombee?"
Aliniambia "nitakupa uwezo huo wa kuongea chochote
ukakubalika bila kupingwa kwa swali lolote" hiyo
iliniduwaza pia nilikubali bila kumpinga. Nilimuuliza babu
kwa kuropoka "babu"
alikuwa tayari anataka kuondoka, akasimama alipokuwa
akitaka kuingia shimoni alipotokea.
"Nataka kufahamu mkuu anasemaje?" akanijibu
"tutazungumza baada ya msiba wangu"
kisha babu alidumbukia shimoni humo. Mzee Nyegezi
alikuja tena chumbani kwangu
aliniuliza kwa ukali "bella umekuwa na tabia gani sasa
hivi?" nilishitushwa na swali hilo mara tu alipoingia.
"kwanini baba" akanijibu kwa hasira "si nilikueleza uamke
ukinge maji"
nilishangaa sana ile hali. Ni kweli mvua ilikuwa kubwa,
lakini cha kushangaza mara tu babu alipotoweka, mvua
ilikatika. Hata lile joto lililonivujisha jasho jingi, likapotea.
Nilimjibu baba
"si imeshakatika?" akaniamba "sasa nataka kesho uamke
mapema ukakinge kwa mama Tunnu" nilimkubalia na yeye
akaondoka. Nililala kwa usingizi wa mang'amung'amu.
..........
Hata asubuhi ilipofika, bado sikujuwa nililala saa ngapi.
Mzee Nyegezi, alikuja mbio chumbani kwangu "Bella
amka... we Bella.. bella" alikuwa amevaa singlendi na
bukta nyepesi. Niliogopa sana. Nilijifuta uso kutoa
tongotongo kwa kiganja cha mkono.
alikuwa ameshika simu "shangazi yako anataka kuongea
na wewe" Baba alikuwa na wasiwasi sana. Ila niliipokea
simu kutoka kwake na kuongea "shikamoo shangazi"
nilichokisikia kutoka upande wa pili, sikutamani kusikia
mara ya pili. Ilikuwa ni sauti ya shangazi akiwa analia.
Alikuwa analia huku akimtaja babu. Ndipo nilipomuuliza
"shangazi kuna nini kwani? Babu kafanya nini?" kwa sauti
ya kilio alinijibu "babu yako amekufaaa Bella" shangazi
aliongea kwa huzuni sana "Bella babu yako Mzee Matonde
amekufa kiajabu mwanangu. Mzee Matonde kipenzi
chako. Kwanini sisi. Kwanini Bellaaaa"
simu iliniponyoka na kudondoka chini. Midomo yangu
ilianza kucheza shere kwa kugongona gongona ya juu
ikaipiga ya chini. Nikabubujikwa na machozi. Mzee
Nyegezi alikuwa akinitazama muda wote, sasa
alinisogelea. "pole Bella" aliniambia kwa sauti iliyopwaya.
mimi nililia sana, kwasababu babu Mzee Matonde hakufa.
Ukweli nilioufahamu kuhusu babu, uliniongezea
machungu. Hicho ndicho kilichoniumiza sana.
nikakumbuka babu alivyoniambia jana usiku "kesho
asubuhi utapokea habari za kifo changu. Hakikisha mwili
wangu hauombewi wala haugwi na watu wengi" ilinibidi
nifanye haraka kuelekea alipokuwa akiishi babu, si mbali
sana na nyumbani; Japo ilinilazimu kupanda gari kwanza.
Mzee Nyegezi naye alitoka chumbani na kwenda
kujiandaa aliniambia "nitaelekea kwanza ofisini, kisha
nitakuja baadaye msibani" nikajibu "sawa" nilizivua nguo
zangu nikajitundika taulo langu safi jeupe. Nikachukuwa
sabuni na kwenda kuchota maji kwenye jaba lililopo jikoni.
Nilipomaliza kujipimia maji niliyoona yanatosha, niliinua
ndoo yangu mswaki mdomoni na kuingia bafuni. Nilianza
kwanza kupiga mswaki. baada ya kumaliza kupiga
mswaki, nikalivua taulo langu na kuliweka pembeni.
Nikausahili mwili wangu kwenye kioo kilichopachikwa
ukutani. Hakika niliumbika. Ukubwa ulioanza
kuninyemelea ukanitunisha mapaja yangu na kuwa
mrembo haswa. Nikatabasamu kidogo kisha nikairudia
ndoo yangu ya maji. Nilichota kopo moja la maji ile
kujimwagia tu usoni, nilianza kuwashwa. Sikuanza
kichwani, kwasababu kama ujuavyo wanawake
kujimwagia maji kichwani kwetu ni sumu. Uso ulianza
kuwashwa sana, mara ukafuatia mwili mzima. Niliwashwa
kupitiliza kama nimejimwagia upupu. Nikawa najikuna
hapa, mara pale. Chini ya matiti yangu, mara mgongoni.
Kucha pekee hazikutosha. Nikajipeleka ukutani. Najikuna
lakini wapi. Muwasho ukazidi. Nikaendelea kuwashwa
zaidi. Muda wote huo sikushituka mapema kama nilikuwa
sioni kitu chochote. Sikujuwa kama macho yangu
yalikuwa yamefumba. Sikujuwa kama nilikuwa nikitembea
kwenye giza nene.

ITAENDELEA!!!
No comments:
Post a Comment