Usipitwe na hizi...


Tuesday, 13 February 2018

Uganda kuchoma dawa 'feki' ; mambo manne yakufahamu kuhusu dawa bandia Afrika

Wizara ya Afya nchini Uganda inaandaa kuteketeza karibu tani 1,500 za dawa ambazo ama zimepitwa na wakati au hazitumiki katika maelfu ya vituo vya serikali nchini Uganda. Tangazo hili limetoka wiki chache baada ya madaktari wa Uganda kugoma huku miongoni mwa madai yao, ukosefu wa dawa hospitalini.
Tatizo la dawa bandia, au dawa zilizopitwa na wakati kuendelea kuuzwa barani Afrika ni kubwa kiasi gani.
Haya ni mambo manne yakufahamu kuhusu dawa bandia Afrika.

1. Idadi ya Vifo inaongezeka

Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani takribani vifo 100,000 vinavyotokea barani Afrika kwa mwaka vinatokana na biashara ya dawa bandia.
Dawa bandia zilizomwagwa katika dampo nchini Ivory Coast kabla ya kuchomwaHaki miliki ya pichaSEYLLOU
Image captionDawa bandia zilizomwagwa katika dampo nchini Ivory Coast kabla ya kuchomwa
Nayo mashirika ya Think-tank nchini Uingereza na mtandao wa serawa kimataifa wameeleza kuwa vifo 700,000 vinavyotokea kwa mwaka vinasababishwa na dawa bandia za kupambana na malaria na kifua kikuu.
2Nchi maskini zinaathirika zaidi
Katika baadhi ya maeneo barani Afrika, Asia na Amerika Kusini,zaidi ya asilimia thelathini ya dawa zilizo sokoni kuuzwa zinaweza kuwa bandia, WHO imeeleza.
Shirika la forodha duniani WCO na Taasisi ya kimataifa ya utafiti dhidi ya dawa bandia, IRACM ilifanya uchunguzi wao katika nchi 16 zikiwemo Kenya, Afrika kusini, Ghana,Senegal na Tanzania.
Wafanyakazi wa Wizara ya Afya, jiijini Abidjan, wakitoa baadhi ya bidhaa wakati wa msako wa dawa bandia nchini humo mwaka 2017Haki miliki ya pichaISSOUF SANOGO
Image captionWafanyakazi wa Wizara ya Afya, jiijini Abidjan, wakitoa baadhi ya bidhaa wakati wa msako wa dawa bandia nchini Ivory Coast mwaka 2017
Takriban dawa milioni 113 zisizofaa na zenye kuhatarisha maisha zilikamatwa barani Afrika,zikiwa na jumla ya thamani ya paundi milioni 52, nchini Nigeria,Benin,Kenya na Togo. Kwa mujibu wa Mkurugenzi mtendaji wa WCO Kunio Mikuriya katika taarifa iliyotolewa mwaka 2017 dawa zote zilizo hatari kwa matumizi ya binaadam na wanyama zimeondolewa sokoni badala ya kuuzwa barani Afrika

3. Watoto ni asilimia kubwa ya wahanga

Mkurugenzi mtendaji wa WHO,Tedros Adhanim amesema tatizo hili linakumba hasa nchi masikini.Kati ya watoto 72,000 na 169,000 hufa kutokana na homa ya mapafu kila mwaka baada ya kutumia dawa bandia.
Dawa nyingi za bandia zinatokea nchini China na kupitishwa katika bandari ya MombasaHaki miliki ya pichaISSOUF SANOGO
Image captionDawa nyingi za bandia zinatokea nchini China na kupitishwa katika bandari ya Mombasa

4. Dawa zinaingilia Afrika Mashariki

Bandari ya Mombasa imeelezwa kuwa ni kitovu cha uingizwaji wa dawa bandia barani Afrika,kama vile dawa za kupambana na malaria na saratani.
Usafirishaji wa dawa bandia unahusishwa kwa karibu sana na matendo mengine ya jinai kama vile utakatishaji fedha na ufadhili kwa makundi ya kigaidi.
Dawa bandia zikiteketea motoHaki miliki ya pichaSEYLLOU
Image captionDawa bandia zikiteketea moto


No comments:

Post a Comment

Pages