Dak ya 84 Yanga wanashambulia kwa kasi na wachezaji wa kagera wanaokoa
Dak ya 82, Kagera wanaumiliki mpira tena, wanajaribu kutafuta bao angalau la kufutia machozi
Dak ya 81 Kagera wanapata Kona, Kipa wa Yanga anaokoa
Dak ya 80 Yanga wanapiga kona nyingine ya 7, Ajibu anapiga Kagera wanaokoa
Dak ya 76, Goooooooli, Martin anaifungia Yanga bao la pili kufuatia krosi nzuri ya Obrey Chirwa, Yanga wana mabao mawili sasa na Kagera 0
Dak ya 76 Yanga wanakosa bao la wazi kabisa, Kagera wanaokoa
Dak ya 72, Omary Daga anaingia kuchuka nafasi ya Atupele Green, matokeo bado ni 1-0
Dak ya 69, Kona wanapata Yanga, ni ya nne na tano katika mchezo wa leo, Ajib anapiga lakini inaokolewa
Dak ya 64, Yanga wanao mpira hivi sasa, Ajib anajaribu kuzunguka lakini ananyang’anywa mpira, Kamusoko anauwahi
Dak ya 55, Kagera wamezidi kuamka licha ya kufungwa bao hilo moja, wanamiliki zaidi mpira eneo la kati
Dak ya 53, Kagera wanaanza upya kati, wanapasiana kuelekea langoni mwa Yanga, inapigwa moja juu, kipa Rostand anaruka kama nyani anaudaka
Dak ya 51, Ajib ndiyo anapiga tuta, anapigaaa, gooooooli, Yanga wanapata bao la kwanza, sasa ni 1-0
Dak ya 51, Penatiiii, Yanga wanapata tuta hapa
Dak ya 46, Beki wa Kagera anachezewa faulo, mpira unapigwa kuelekea langoni mwa Yanga
Dak ya 45, Kipindi cha pili kimeanza, matokeo ni 0-0
MAPUMZIKO
Kipindi cha kwanza kimekamili.
45′ Zinaongezwa dakika mbili za nyongeza.
43′ Kipa wa Kagera Sugar yupo chini anatibiwa. Mchezo umesimama.
40′ Timu zinashambuliana kwa zamu.
35′ Kagera wanapata kona inapigwa.
33′ Yanga wanamtoa Pato Ngonyani, anaingia Maka.
29′ Kagera wanaonyesha utulivu.
28′ Mchezo umechangamka, timu zote zinapeana zamu kumiliki mpira.
25′ Chirwa anachezewa faulo na Kavila.
25′ Yanga ndiyo ambao wanamiliki mpira na wanaonyesha kucheza kwa kasi.
22′ Ajibu anapiga faulo inapaa juu ya lango.
21′ Gereza wa Kagera anapata kadi ya njano kwa kucheza faulo, Yanga wanapata faulo.
18′ Kibaya wa Kagera anapata kadi ya njano kwa kuonyesha mchezo mbaya dhidi ya Kelvin Yondani.
14′ Yanga wanafanya shambulizi kali, Buswita anaonyesha makali lakini kipa wa Kagera anauwahi mpira.
11′ Yanga wanapata kona. Ibrahim Ajibu anapiga lakini kipa wa Kagera anauwahi mpira na kuudaka.
10′ Kamusoko anaonyes uhodari wa kumiliki mpira.
9′ Atupele Green wa Kagera anapata nafasi lakini anakosa umakini.
8′ Timu zote zinasomana, Yanga wanamiliki mpira na kupiga pasi nyingi.
4′ Kasi ya mchezo siyo kubwa.
1′ Mchezo umeanza.
Timu zinaingia uwanjani.
Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment