Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas (katikati) akiwa na washindi.
KAMPUNI ya michezo ya kubashiri nchini ya SportPesa Tanzania imekabidhi shilingi milioni 12 kwa washindi 12 wa Promosheni ya Shinda na SportPesa.
Washindi hao 12 walijishindia tiketi za kwenda nchini Uingereza kushuhudia mechi ya Ligi Kuu nchini huko kupitia promosheni hiyo, lakini kutokana na sababu mbalimbali wameshindwa kusafiri hivyo kila mmoja alikabidhiwa shilingi milioni moja kama fidia ya safari hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas alisema “Kampuni yetu ina ushirika na klabu mbalimbali kama mshindi atapata nafasi ya kwenda kushuhudia mechi atapata nafasi ya kutembelea makao makuu ya klabu hizo ikiwemo Arsenal na Everton.
“Kutokana na vigezo na masharti vya promosheni hizi mbili, hatutawaacha washindi wetu mikono mitupu bali kila mmoja wao ataondoka na kiasi cha shilingi milioni moja ambazo watazitumia wapendavyo, na hii ni kwa mujibu wa masharti ya promotion hizo.”
Akizungumza kwa niaba ya washindi wenzake, Musa Yohana alisema kuwa “Kwanza kabisa napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa kampuni ya SportPesa, mimi ni mshindi niliyepatikana kupitia promosheni ya Shindana SportPesa.
“Kutokana na shughuli zangu binafsi niliomba kutosafiri na kuitaka kampuni inilipe fedha badala ya safari kama kanuni na masharti ya promosheni yanavyoelekeza,”alisema Yohana.
mwisho
No comments:
Post a Comment