STORY YA UKWELI: SAFARI YA UZIMUNI (SEHEMU YA KWANZA)
Kwa sasa naishi Mbagala, jijini Dar es Salaam na familia yangu yenye mke na watoto saba, wote wa kike. Mke wangu pia kwao ni mtoto wa kwanza katika familia yenye watoto tisa, wote wanawake.
Nimelazimika kusimulia mkasa huu wa kichawi baada ya watu wengi kusimulia mikasa yao wakidai waliwahi kuwa wachawi wakaacha kwa sababu mbalimbali ambazo wengine huzisema, wengine hufanya siri kubwa.
Naweza kusema kwamba, karibu wote waliokuwa wakisimulia maisha yao ya kichawi na mikasa yake, hakuna hata mmoja aliyewahi kufikia hata robo ya maisha ya kichawi ya kwangu.
Naweza kusema kwamba, karibu wote waliokuwa wakisimulia maisha yao ya kichawi na mikasa yake, hakuna hata mmoja aliyewahi kufikia hata robo ya maisha ya kichawi ya kwangu.
Mimi niliishi maisha hayo kwa miaka kumi, na nilifika ‘levo’ ya mbali, mfano kuwa Mkuu wa Kikundi na kusafiri sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya mikutano mikubwa ya kimataifa ya wachawi na niliporudi, nilikuwa nakutana na wachawi wakubwa wa hapa nyumbani Tanzania na kuwapa maagizo ya utendaji katika makundi yao sehemu mbalimbali za nchi.
Katika kipindi chote cha kuwa mchawi nilibaini mambo makubwa mawili, kwamba, maisha ya wachawi katika ulimwengu wao hayana tofauti yoyote na maisha ya watu wasio wachawi katika ulimwengu huu wa macho ya kawaida.
Maandiko yanaposema kuwa, Mungu aliumba vitu vinavyoonekana na visivyoonekana ni kweli kabisa. Wachawi wanaamini kwamba, vitu visivyoonekana pia vilikuwa na siku sita katika uumbaji wa Mungu, siku ya saba akapumzika. Na hiyo ndiyo sera ya mchawi mara tu baada ya kujiunga katika kazi hiyo inayolaaniwa na wengi ulimwenguni kote.
Kabla sijaenda mbele zaidi nataka kusema kuwa, kama kuna shughuli mbalimbali za binadamu zinazoonekana kwa macho ya kawaida duniani, pia kuna shughuli kama hizo hizo zisizoonekana kwa
Wachawi wana kila kitu, wana mikutano ya nchi, mikutano ya kimataifa, ya kanda ya mabara na pia wana mabenki, japokuwa kwa macho tunazungumzia mabenki ya pesa, wao wana mabenki ya damu, nyama na dawa za kienyeji.
Itaendeleea………………………………………….
No comments:
Post a Comment